January 3, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amefika katika
kijiji cha Tindiga kilichopo wilaya ya Mikumi zilipotokea vurugu
zilizopelekea mkulima mmoja kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni
na kusikiliza kero zinazowasumbua wananchi wa Kilosa kabla ya kutoa
maamuzi.
Waziri Mwigulu amesema kuanzia sasa likitokea tukio lolote la watu
kuuana kwa mapanga, mikuki, sime na silaha zozote za jadi zinazotumiwa
hasa na wakulima na wafugaji, serikali itafuta utaratibu wa kubeba
silaha hizo na atakayebeba atakamatwa na kuchukuliwa hatua kama
watuhumiwa wengine.
Kinginie alichoagiza Waziri Mwigulu ni wakuliam na wafugaji kwa pamoja
kuwakamata watu wote watakaohusika na kuanzisha vurugu na kuwafikisha
kwenye vyombo vya dola kabla jeshi la polisi halijafanya maamuzi yake.
“Kuanzia leo tunaanza kuhesabu pakitokea tukio lolote la vurugu na
zikatumika silaha kuwadhuru wananchi, tutafuta utaratibu wa watu
kutembea na silaha mitaani, na ukikutwa nayo unakamatwa kama ambavyo mtu
mtu mwenye silaha ya moto na hajaiandikisha. Hatuwezi kuruhusu hii
ikawa nchi ya watu wanakatanakatana tu” – Waziri Mwigulu Nchemba
Home / featured /
kitaifa
/ MAAMUZI mapya ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu mauaji ya wakulima na wafugaji
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.