Msanii wa bongo fleva Darasa ameweka wazi ule mstari wake wa "sio simba,
sio chui, sio mamba" kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani
simba ni mnyama ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.
Akipiga story kupitia eNewz Darasa amesema Diamond ni msanii ambaye
amehangaika sana kutoka kimuziki hivyo mafanikio yake na uwezo wake wa
muziki alitakiwa ajiite jina lingine kwa kuwa Daimondi ni zaidi ya Simba
kwa sasa kwani ni zaidi ya mnyama Simba.
"Ningekuwa Diamond nisingejiita simba, ninavyomuona Diamond ni zaidi ya
Simba, kuna watu wanaua simba, simba, kajichanganya, kaingia kijijini
kapotea, Diamond kwa kitu anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza
kujiita jina lingine lolote kubwa, kafanya vitu vingi sana". Amesema
Darassa
Darassa amemalizia kwa kusema wanyama wote ambao amewataja katika wimbo
wake hawaogopi kwa kuwa ana kitu kikubwa ndani yake na yeye ni mwanaume
na anajiamini kwa muziki wake anaofanya.
"Kwa upande wangu nimesema siyo simba, siyo chui siyo mamba, mamba ni
mnyama anayetisha sana kwenye maji, simba anatisha sana porini, chui ni
hunter mzuri, so katika vitu vyote ambavyo viko humo, mimi humo kote
simo, ninacho kitu ambacho kinaweza kunifanya nikwambie aaaaah".
Amemalizia Darassa
MWANAMUZIKI Darassa Afunguka "Diamond Hapaswi Kujiita Simba"
darasa
,
entertainment
,
featured
,
simba
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.