latest Post

Simba ruksa kuwatumia Wakimataifa Kesho

Uongozi wa Simba chini ya Katibu Mkuu Patrick Kahemela umepambana na kufanikiwa kupata vibay hivyo ambavyo sasa vinawaruhusu kuwatumia nyota hao kuanzia mchezo wa kesho dhidi ya...
Hatimaye klabu ya Simba, imefanikiwa kuwapatia vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini makocha na wachezaji wake wa kigeni na kehso wanaweza kuwatumia katika mechi yao ya ligi ya Vodacom dhidi ya JKT Ruvu.
Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele ameiambia Goal, kwamba watu hao kwasasa wapo huru na wanajisikia faraja kuona jambo hilo wamelikamilisha kwa haraka kama ilivyohitajika.
“Tunafuraha kuona tumekamilisha taratibu zote zilizohitajika wachezaji na makocha wote tunatarajiwa kuwatumia katika mchezo wa kesho dhidi ya JKT Ruvu, ambao utachezwa uwanja wa Uhuru, na kizuri nikwamba tunauhakika wa kuendeleza ushindi baada ya kikosi kukamilika,”amesema Kahemela.
Kiongozi huyo amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kutokana na hali hiyo kujitokeza na kuwavuruga vichwa kutokana na mapenzi yao kwa Simba, lakini hivisasa mambo yote yapo sawa na watarajie kupata pointi nyyingine tatu hiyo kesho.
Nani kafanya usajili bora zaidi katika dirisha dogo la usajili?
Amesema swala hilo limewapa funzo kubwa na watajitahidi kuhakikisha wanalifanyia kazi kila ambapo watasajili mchezaji au kuchukua kocha mpya ili kuepuka mambo kama hayo.
“Ukweli yametufunza na tusingependa hili lijitokeze tena kwasababu nikama linaidhalilisha klabu na wachezaji wenyewe wakigeni ambao sisi ndiyo tunahusika kwa ujio wao hapa nchini,”amesema Kahemela.
Aidha kiongozi huyo amesema klabu yao ipo kwenye mikakati kabambe, ya kuhakikisha hapaondoki kwenye kiti cha uongozi wa ligi hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu.
Amesema mipango yao ni kuhakikisha kila mechi wanacheza na kupata ushindi ambao utawapo pointi tatu na kuendelea kuongoza kama ambavyo wamepanga iwe.
Wachezaji na makocha ambao walipigwa stopu na Kamati ya Uhamiaji ni Kocha Mkuu, Mcameroon, Joseph Omog, Mganda Jackson Mayanja kocha Msaidizi, Kocha wa makipa, Mkenya Idd Salim na wachezaji Janvier Besala Bokungu kutoka DRC, Method Mwanjali kutoka Zimbabwe, Daniel Agyei, James Kotei kutoka Ghana, Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast na Laudit Mavugo kutoka Burundi.

About Good Sensei

Good Sensei
Recommended Posts × +

Entertainment

Latest News

Pictures