Pamoja na uwepo wa matatizo ushindi ndio kila kitu kutokana na melengo tuliyokuwa nayo msimu huu
Lwandamina ameiambia Goal, wachezaji wake wote wapo sawa na wamemuahidi ushindi kutokana na hamasa waliyokuwa nayo katika kupigania kurudi kileleni mwa msimamo.
“Nikweli tumekosa mazoezi kwa siku mbili lakini kitu cha kufurahisha vijana wote wapo sawa kwa ajili ya mchezo wa leo jioni na wameniahidi ushindi kitu ambacho kimenifurahisha,”amesema Lwandamina.
Kocha huyo amesema wanalazimika kusahau matatizo yao na kuweka mbele kazi kwasababu hayo ni mambo ya mpito ambayo hayapaswi kukaa kwenye vichwa vyao kwa muda mrefu.
Conte: "Kuwakosa Costa na Kante ni mtihani Chelsea"
Amesema matokeo ni jambo muhimu katika kila mchezo ili kuifukuzia nafasi ya kwanza ambayo ndiyo inalengo jema la kubeba ubingwa wa msimu huu na kuwapa presha wapinzani wao Simba ambao kwasasa ndiyo wanaongoza ligi.
“Unajua mambo ya migomo, hayana nafasi kwa kipindi hiki hayo yalishapita na jambo la msingi kwetu ni kuona Yanga inafanya vizuri kwa kupata matokeo kwenye mechi zake ikiwemo ya leo ndiyo maana wachezaji wamesahau hayo na kuahidi ushindi kwenye mchezo wetu wa leo na Afrcan Lyon, amesema Lwandamina.
Kocha huyo amesema akili na mikakati yao kwa sasa ni kuangalia ni jinsi gani timu hiyo inabadilika katika kila mchezo na kuwafurahisha mashabiki wao ambao wangependa kuiona timu hiyo ikipata matokeo mazuri na kutwaa ubingwa kwa mara nyingine.
Mzambia huyo amesema pamoja na wachezaji wake kumhakikishia ushindi lakini wataingia kwa tahadhari kubwa kwakua ameambiwa rekodi za timu hiyo msimu huu kwa kuifunga Simba na kutoka sare mechi mbili dhidi ya Azam FC.
Katika mchezo wa leo Yanga itamkosa mshambuliaji wake Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano kwenye mechi zilizopita hivyo Amissi Tambwe anatarajiwa kuongoza mashambulizi pamoja na Mzambia Obrey Chirwa.