latest Post

Omog atamuweza Bakari Shime Kesho?

Ni mchezo ambao unaweza kukwamisha mipango ya Simba kama itashindwa kupata ushindi kutokana na rekodi za timu hiyo katika siku za karibuni
Kikosi  cha Simba kinachonolewa na kocha Joseph Omog, kesho kitakuwa nyumbani Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, kuwakabili maafande wa JKT Ruvu, katika mchezo wa ligi ya Vodacom mzunguko wa 17.
Simba ambayo inaongoza ligi, itakuwa inapambana kutafuta kujiongezea heshima ya kuongoza ligi endapo itashinda mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote mbili.
Ikumbukwe Simba ndiyo vinara wa ligi hiyo baada ya kujikusanyia pointi 38, katika michezo 16, waliyocheza wakati wapinzani wao JKT Ruvu, wanashika nafasi ya tatu kutoka mwisho wakiwa na pointi 13 walizovuna kwenye mzunguko wa kwanza.
Simba itaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa inajivunia ushindi wa mabao 2-0, iliyoupata Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara, wakati JKT Ruvu yenyewe watakao kuwa wageni watakuwa wanakumbuka kipigo cha mabao 3-0, kutoka kwa mabingwa watetezi Yanga.
Mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa mgumu hasa kwenye eneo la kiungo ambalo litawakutanisha wachezaji wenye uwezo mkubwa kama Jonas Mkude na Mohamed Ibrahim ‘MO’ kwa upande wa Simba wakati kwa JKT Ruvu yupo Hassan Dilunga na Yohana Nkomola.
Kocha Joseph Omog anatarajia kukitumia kikosi chake kamili, ambacho kina mastaa wote wakiwemo wachezaji wa kigeni ambao tayari wamepata vibali vya kufanya kazi na kuishi Tanzania baada ya siku tatu zilizopita kupigwa stop na idara ya uhamiaji.
Mshambuliaji Laudit Mavugo na Fredrick Blangon wanatarajiwa kuongoza mashambulizi ya timu hiyo sambamba na kiungo mpya James Kotei, ambaye alicheza kwa dakika 13, katika mchezo uliopita na kutolewa nje baada ya kuumia.
Kipa Daniel Agyei raia wa Ghana ataanzia langoni huku akilindwa na nahodha Method Mwanjali na Novaty Lufunga ambao watakuwa wanasaidiana na Mohamed Hussein ‘Zimbwe’ na Jamvier Bukungu.
Kocha Omog, ametamba kuwa kukosi chake kipo katika hali nzuri na wanatarajia kucheza kwa kushambulia zaidi kesho ili kupata ushindi ambao utawafanya kuendelea kuongoza ligi kama walivyopanga iwe hivyo hadi mwishoni mwa msimu .
Mcameroon huyo amesema atampa nafasi mshambuliaji mpya Juma Luizia ambaye amemsajili kwa mkopo kutoka Zesco United ya Zambia kwenye dirisha dogo, na mfumo atakao utumia ni ule wa 4-4-2 ambao amekuwa akiuaminia kutokana na kupata ushindi katika mechi zilizopita.
Mshambuliaji Ibrahim Ajibu anatarajiwa kuanzia benchi sambamba na nahodha Jonas Mkude ili kutoa nafasi kwa Kotei, kuanza kikosi cha kwanza ili kuweza kuizoea ligi na kujitambulisha kwa mashabiki kutokana na kucheza nyumbani.
Kwupande wake kocha Bakari Shime wa JKT Ruvu huo ni mtihani wake wa pili tangu kuichukua timu hiyo na analazimika kushinda ili kuinusuru timu hiyo isiweze kuzidi kujiweka kwenye mazingira magumu ya kushuka daraja.
Shime anajivunia kiwango bora ambacho vijana wake walichokionyesha kwenye mchezo wao na Yanga na kusema makosa yaliyosababisha wakafungwa mabao 3-0 na Yanga hayatojirudia tena badala yake watapambana ili kupata ushindi.
Pamoja na JKT Ruvu, kutopewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo lakini rekodi zinaonyesha kuwa Simba imekuwa katika wakati mgumu inapokutana na Maafande hao na katika mechi nne zilizopita Simba haijawahi kupata ushindi zaidi ya kulazimishwa sare na kupoteza mchezo kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mchezo wa mwisho kukutana kwenye uwanja wa Taifa timu hizo zilikwenda sare ya bila kufungana matokeo ambayo yalififisha matumaini ya Simb, kabla ya kujipanga upya na kushinda mechi zao zilizofuata hadi kufanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni.
Kipa Said Kipao, Edward Charles Michael Aidan wanatarajiwa kuweka ulinzi imara wa timu hiyo huku Atupele Green na Saad Kipanga wakiwa na kazi moja ya kuongoza mashambulizi kwenye lango la Simba wakitaka kumfunga kipa Agyei.

About Good Sensei

Good Sensei
Recommended Posts × +

Entertainment

Latest News

Pictures