Jose Mourinho ameanza kuulalamikia uchezaji wa
Chelsea kukaba kwa nguvu akidai sababu hiyo itaifanya United isishinde
ubingwa wa ligi
Man United inayoshika nafasi ya sita ipo nyuma ya Chelsea kwa jumla ya pointi 13, ambao wameshinda mechi zao 11 za mwisho na kuizidi Liverpool inayoshika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi sita.
Mourinho amefunguka kuwa haitakuwa rahisi kwa klabu yake mpya kuziba pengo hilo la alama dhidi ya klabu yake ya zamani, hasa ukizingatia Chelsea wanacheza mchezo wa kukaba zaidi.
“Ni vema kuwa mkweli na kusema kwamba ni ngumu sana (kutwaa ubingwa msimu huu). Si tofauti ya alama tu, bali pia falsafa ya Chelsea katika uchezaji. Hawajali nini watu wanasema, wala wanachofikiria watu. Wao wanataka kushinda tu. Na kwa sababu hiyo, sidhani kama watapoteza pointi.”
Mechi nne za mwisho kati ya sita walizoshinda Chelsea Ligi Kuu wamepata ushindi wa 1-0.
Man United yapigana vikumbo na Arsenal kumpata Payet
Manchester United wameonesha nia ya kupambana na Arsenal kuiwania saini ya Dimitri Payet katika dirisha la uhamisho la Januari.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa inasemekana anataka kuondoka kwenye timu yake ya sasa West Ham United na ameongea na chombo cha habari cha Ufaransa RMC Sport kuhusu kucheza kwenye klabu nyingine.
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger inaeleweka dhahiri kuwa anavutiwa na uwezo wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, lakini The Sun limedai kuwa Jose Mourinho naye amejitosa katika mbio za kumfukuzia mshambulizi huyo.
West Ham ambao kwa sasa wapo kwenye hatari ya kushuka daraja Ligi Kuu Uingereza walimsajili Payet kutokea Marseille kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 10.7 mwaka 2015.