latest Post

Kally Ongalla: "Lazima Tuwafunge Azam Kesho

Nimchezo mgumu kwa timu zote kwani zinahitaji ushindi ili kujiimarisha katika nafasi zao ingawa wenyeji Majimaji wana hali mbaya zaidi
Majimaji FC, kesho itakuwa nyumbani Uwanja wa Majimaji kuwaalika Matajiri wa Azam FC, katika mchezo wa ligi ya Vodacom kesho saa 10:00 jioni.
Wenyeji Majimaji hawapo kwenye nafasi nzuri sana baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza kwenye nafasi ya 11, wakiwa na pointi 15 na mchezo uliopita walijikuta wakipoteza nyumbani mbele ya Tanzania Prisons ya Mbeya.
Azam imekwenda Ruvuma ikipania kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini ya kuzifukuzia Simba na Yanga zilizopo kwenye nafasi mbili za juu na hiyo ni baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na  African Lyon mchezo uliopita.
Kocha wa Majimaji Kally Ongalla, amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo ambao amesema utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu wanayocheza nayo .
“Nimchezo mgumu lakini tunajivunia kuwa nyumbani tunataka kuwafurahisha mashabiki wetu hivyo hatuta kubali kufungwa kwa mara ya pili tunataka kutoka hapa tulipo ili kwenda mbali zaidi,”amesema Ongalla.
Majimaji imeongeza wachezaji watatu kwenye dirsha dogo mmoja wapo akiwa ni mkongwe Mbuyu Twite aliyekuwa akiichezea Yanga, na anaweza kuwa na msaada mkubwa mchezaji huyo kutokana na uzoefu aliokuwa nao.
Kwaupande wao Azam tayari wameshafika Ruvuma kwa ajili ya mchezo huo na msemaji wa timu hiyo Jafari Idd, amesema timu yao ipo katika hali nzuri na wamejiandaa kuhakikisha wanashinda pambano hilo.
Amesema wamekwenda na kikosi chao kamili na wataingia kwenye mchezo huo kwa nguvu kubwa kuhakikisha wanapata ushindi wa mapema utakao punguza gepu kati yao na vinara Simba.
“Hatukufanya vizuri kwenye mchezo wetu wa raundi 16, dhidi ya African Lyon, sasa tumejipanga kuona tunazindukia tukiwa huku Ruvuma, najua mchezo utakuwa mgumu kwasababu wenyeji wetu wapo nyumbani na hawatapenda kufungwa tena wakiwa nyumbani,”amesema Idd.
Kiongozi huyo amesema kocha wao Zeben Hernandez, amemhakikishia ushindi baada ya kikosi chao kufanya maandalizi ya kutosha baada ya mchezo wao uliopita na wachezaji kuelewa mfumo ambao wanatakiwa kuutumia hivyo amewatoa presha mashabiki wao na kuwataka wasubiri pointi tatu.
Amesema kusudio lao kubwa ni ubingwa msimu huu na harakati hizo wangependa zianzie kwenye mchezo huo ambao wameupa umuhimu mkubwa kwani wanaamini kama watashinda mchezo huo utawarahisishia hata mechi zinazofuata ziwe nyepesi kwao.
“Unajua ushindani umekuwa mkubwa hakuna timu ndogo, na kwenye kikosi chetu tunawachezaji wengi wageni hicho ndiyo kilitusumbua na kushindwa kupata bao kwenye mchezo uliopita lakini tunaamini mchezo wetu wa kesho dhidi ya Majimaji utakuwa na mabadiliko tusubiri kuona,”amesema Idd.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex wenyeji Azam walishinda mabao 3-0.

About Good Sensei

Good Sensei
Recommended Posts × +

Entertainment

Latest News

Pictures