Yanga wanategemea sana mipira ya pembeni, sasa tulijaribu kuangalia watu
wanaowachezesha wale watu wa pembeni, tukawakamata na ukiwakamata Yanga
kwenye midfield basi unakuwa umeua plan zao wakaishiwa maarifa wakawa
hawajui nini cha kufanya sisi tukawa tunatengeneza nafasi na kuzitumia,”
anasema kocha wa muda wa Azam Idd Cheche baada ya kuiongoza timu yake
kupata ushindi wa kihistoria dhidi ya Yanga.
Kwenye michezo miwili iliyopita Azam haikuonesha kiwango kizuri
kiuchezaji huku washambuliaji wake wakishindwa kutumia vizuri nafasi,
Cheche amesema tatizo lilikuwa ni umaliziaji na walilifanyia marekebisho
ndio maana safu ya ushambuliaji ilikuwa hatari dhidi ya Yanga.
“Tumerekebisha safu ya shambuliaji ndio ilikuwa inasumbua kidogo,
tulikuwa tunapata nafasi lakini tuikuwa tunashindwa kuzitumia, movements
zilikuwa ndogo kwa hiyo tumelifanyia kazi hili suala la finishing ndio
limeleta haya matunda yaliyotokea.”
Azam imefuzu hatua ya nusu fainali na inatarajia kukutana na timu
itakayomaliza nafasi ya pili kutoka Kundi A lenye timu za Simba, Taifa
Jang’ombe, Jang’ombe Boys na URA ambazo zote zina nafasi.
Hii ndio kauli ya Cheche kuelekea mechi ya nusu fainali: “Yoyote
atakaekuja kwenye nusu fainali atakuwa ni mzuri na sisi tumejiandaa
kupambana nae tuhakikishe tunavuka tunaingia fainali na kuchukua kombe.”
Home / Azam /
featured /
kitaifa /
michezo /
Yanga
/ Kocha wa Azam Ameitaja Sehemu Alipoikamata Yanga
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.