Arsenal watasafiri kwenda Manchester Jumapili jioni
kwenda kuikabili City katika dimba la Etihad, Wenger anaamini sasa
wanaweza kuchuana na City
Arsenal walipoteza idadi kubwa ya wachezaji kwa City katika kipindi cha miaka mitano, ikiwa ni pamoja na Bacary Sagna, Kolo Toure, Gael Clichy, Samir Nasri na Emmanuel Adebayor.
Arsenal hawakuwa na uwezo wa kushindana na City kifedha kwa maana ya mishahara ya wachezaji na fedha za uhamisho katika miaka ya 2009 na 2014, lakini Wenger amesisitiza kuwa kutorokwa na wachezaji sasa basi, amesema hayo kufuatia tetesi kuwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez huenda wakatua Etihad majira ya joto.
“City walikuwa wateja wazuri!” aliwaambia waandishi kuelekea mechi itakayowakutanisha Arsenal na Manchester City. “Tupo imara sasa kwa sababu sasa naamini tunaweza kukidhi haja zetu za kifedha na kuwawezesha wachezaji kupata matakwa yao na kuwafanya waifurahie klabu.
“Hapo awali, tofauti ya kifedha ilikuwa kubwa kiasi cha kushindwa kubakisha wachezaji wetu. Hatukuweza kuchuana, tulilazimika kuwauza wachezaji. Kiasi fulani hali hiyo imepungua ingawa bado ipo.”
Inaeleweka kuwa Sanchez amepewa kitita cha paundi 400,000 kwa wiki kujiunga na klabu ya Chinese Super League, wakati Ozil anatakiwa na timu kadhaa za Ulaya.
Manchester City inasaka kipa mpya majira ya joto
Manchester City wameripotiwa kuwa kwenye mchakato wa kuandaa dau la paundi milioni 20 kwa ajili ya kipa wa Kibrazili Ederson Moraes msimu ujao wa majira ya joto.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa anakipiga katika klabu ya Benfica inayoshiriki Ligi Kuu ya Ureno na meneja wa Manchester City Pep Guardiola anamtaka kumwongezea changamoto Claudio Bravo.
Bravo alitua City majira ya joto akitokea Barcelona baada ya Guardiola kuonekana kutokubali uwezo wa Joe Hart na kumtoa kwa mkopo Torino.
Kwa sasa anatarajiwa kuuzwa majira ya joto na inaaminika bei yake tajwa ni paundi milioni 10 kwa klabu za kigeni na angalau paundi milioni 20 kwa klabu za Ligi ya Uingereza.
Moraes alitua Benfica kwa dili la paundi 425,000 akitokea Rio Ave mnano 2015 na kufanikiwa kutwaa taji la Primera Liga na Taca de Portugal katika msimu wake wa kwanza klabuni.