latest Post

Nyota wapya wa Azam hoi kwa African Lyon

Pamoja na kukimbiwa na wachezaji wengi kwenye dirisha dogo la usajili lakini African Lyon waliweza kuhimili presha za Azam na kuambulia sare hiyo
Mwenyekiti  wa klabu ya Azam FC, Idrissa Nassoro, amesema pamoja na kikosi chao kushindwa kupata ushindi dhidi ya African Lyon hapo jana lakini bado wana matumaini ya ubingwa msimu huu kutokana na usajili walioufanya kwenye dirisha dogo.
Nassoro ameiambia Goal, kuwa timu yao ilicheza vizuri na kushambuliazaidi ya wapinzani wao lakini walikosa bahati ya kufunga ndiyo maana mchezo huo ukamalizika kwa sare ya 0-0.
“Hakuna wa kumlaumu zaidi ya kuwapongeza wapinzani wetu kwa mbinu zao kuwasaidia kupata pointi moja lakini tuliwashambulia sana na kila mchezaji alifanya kazi yake vizuri lakini bahati haikuwa yakwetu na hayo yanatokea kwenye mchezo wa soka,”amesema Nassoro.
Kiongozi huyo amesema baada ya kumalizika mchezo huo anaimani kocha wao Mhispania Zeben Hernandez, atakuwa ameona mapungufu yaliyokuwepo na watayafanyia kazi ili kufanya vizuri kwenye mechi zinazofuata za ligi hiyo.
Amesema matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu bado yapo palepale hivyo wataendelea kupambana na wao kama viongozi kuwapa motisha wachezaji ili kuhakikisha wanatimiza lengo lao la kutwaa ubingwa msimu huu.
“Tunafahamu kuwa ushindani ni mkubwa na sare ya Lyon imeongeza gepu kati yetu na timu mbili za juu, lakini hatuwezi kukata tamaa kwasabnabu ligi bado nindefu na chochote kinaweza kutokea mbele ya safari lakini kwasasa bado tunazo ndoto za ubingwa kwasababu uwezo wa kufanya hivyo tunao,”amesema.
Kiongozi huyo amesema anafahamu wanakazi ngumu katika mchezo ujao dhidi ya Majimaji, watakayocheza nayo Desemba 24, mkoani Ruvuma, lakini wanakwenda huko wakiwa wamejipanga kuhakikisha wanavuna pointi tatu ambazo zitawarudisha kwenye ushindani uliopo hivi sasa.
Sare hiyo dhidi ya Lyon imeifanya Azam kuwa nyuma kwa pointi 13 dhidi ya vinara Simba wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 38 wakifuatiwa na Mabingwa watetezi Yanga wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 36.

Azam ndiyo timu iliyoongoza kwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa kusajili nyota sita wapya wakiwemo watano wa kimataifa lakini walishindwa kupata matokeo mbele ya Lyon ambayo ilikuwa dhaifu kuliko ilivyokuwa mzunguko wa kwanza.

About Good Sensei

Good Sensei
Recommended Posts × +

Entertainment

Latest News

Pictures