Baada ya headlines katika mitandao ya kijamii kuhusiana msanii wa Bongofleva Young D ambaye kwa sasa ameziteka Tv&Radio Stations nyingi kutokana na wimbo wake ‘Furaha’,
kudaiwa kumtelekeza mtoto wake, December 10 2016 ametumia account yake
ya instagram kuelezea ukweli wa ishu hiyo na kusikitishwa kwake.
“Nawashukuru sana watu wote ambao wamekuwa waki-support kazi yangu mpya #Furaha Either
Naomba radhi kwa mashabiki zangu ambao wamekwazika kwa njia moja au
nyingine kutokana na taarifa za uongo zilizosambaa mtandaoni”
“Ikumbukwe tarehe 22 June
mwaka huu niliitisha press nikaomba radhi kwa waTanzania na mashabiki
zangu wote kwa ujumla, nikaeleza kuwa nimepitia kipindi kigumu sana na
kuwa kuna mengi nimefanya ambayo sijivunii na najutia”
“Niliahidi
kubadilika na kuwa mfano mzuri kwa jamii. Kwa kipindi kirefu nimekuwa
nikipigana na nafsi yangu kuhakikisha sirudii makosa. Madhara
yanayotokana na matendo niliyofanya kipindi kile hadi leo bado
yananitafuna ila nimekuwa nikijitahidi kukabiliana nayo”
“Nilipewa taarifa na mamisa kuwa ana mimba yangu ya (miezi 6),
kama kijana nilishtuka na kupata ugumu kuikubali hali hiyo kutokana na
kwamba nilikua nimetoka kwenye kipindi kigumu. Baada ya kutafakari
nilimuomba aitunze hiyo mimba asiitoe!!! Kama ni mwanangu ntamlea. Kama
ningekuwa na nia ya kumkana mtoto au kumtelekeza, kwanini nimwambie
asitoe?”
“Si
kutaka kumshirikisha mtu kwanza bila kuwa na uhakika kwamba kweli mtoto
ni wangu. Management yangu sikuishirikisha kwa lolote kwa sababu
inanisaidia sana katika kuhakikisha career yangu ya music ina imarika.
Hivyo nilihisi ni taarifa ambayo inaweza kui-disappoint na kukatisha
malengo. Hata familia yangu Mama, dada na ndugu sikuwaeleza kitu.
Nilitaka nijipange vizuri, nijihakikishie kweli mtoto ni wangu, nitafute
njia sahihi ya kueleza hili jambo”
“Nimesikitika sana kuona kuwa sio kila mtu anafurahia
unapofanikiwa, unapoamua kufanya kazi ili upate maendeleo. Wapo watu
ambao bado watatafuta fursa ya kukuharibia maisha. Yote kheri Namuachia
mungu baba. Mtoto wangu nimempokea kwa moyo mmoja. Ni mtoto wa kike, na
anaitwa Tamar”
“Nimewataarifu
ndugu na wazazi wangu kuhusu hili, nashukuru wamenielewa. Nimeuelewesha
pia uongozi wangu, wamenielewa. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa
Kumjaalia uhai mwanangu, amezaliwa akiwa salama kiafya. Shukrani za
dhati ziende kwa uongozi wangu, kwani wamekua wakihakikisha nasimama
katika njia sahihi bila kuyumba. Shukrani kwenu SHILAWADU kwa kujaribu
kuzirudisha nyuma jitihada zangu za kimaendeleo. #YoungDaddy“
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.