latest Post

Timu 5 zilizotumia pesa nyingi usajili dirisha Dogo

Timu tatu za juu zinazofukuzia ubingwa Simba, Yanga na Azam ndizo zimetumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao kabla ya duru la pili kuanza
Timu tatu za juu zinazo fukuzia ubingwa Simba, Yanga na Azam ndizo zinazoonekana kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao kabla ya duru la pili kuanza Jumamosi ya Desemba 17.
Matajiri wa Azam ndiyo wanaoongoza kwa timu zote 16, zinazoshiriki ligi ya Vodacom kwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa kusajili ikifuatiwa na Simba na mabingwa watetezi Yanga wanashika nafasi ya tatu.
Goal, inatambua kuwa Azam baada ya kufanya vibaya mzunguko wa kwanza imevunja benki na kutumia zaidi ya bilioni 1.2 kusajili wachezaji watano wapya wakiwemo raia watatu wa Ghana mmoja wa Cameroon na Mtanzania mmoja.
Wachezaji hao ni Stephan Kingue Mpondo kutoka Cameroon, Yakubu Mohammed, Samwel Afful, Daniel Amoah na Samuel Agyei  kutoka Ghana na mwingine ni mzalendo Joseph Mahundi.
Gharama hizo zinatokana na fedha za usajili wa wachezaji hao  kutoka timu walizokuwa wanazichezea  pamoja na mishahara yao kwa mwezi kitu kinachoifanya klabu hiyo kuwa ndiyo kinara kwa kulipa mishahara mikubwa wachezaji wake.
Azam wamewasajili wachezaji hao wanne na kuamua kuvunja mikataba ya waliokuwa nyota wao wanne pia ambao ni Michael Balou, YA Thomas, na Pascal Wawa wote raia wa Ivory Coast na mwingine ni Mnyarwanda Baptiste Mugiraneza
Simba ambao ndiyo vinara wa ligi ya Vodacom kwenye mzunguko wa kwanza wenyewe hadi kufikia leo wametangaza kusajili nyota watatu wapya kipa Daniel Agyei, James Kotei wote raia wa Ghana na Watanzania wawili wanaocheza nafasi ya ushambuliaji Pastory Athans na Juma Luizio, aliyekuwa akicheza Zesco United ya Zambia.
Usajili huu unakadiriwa kutumia milioni 350 za kitanzania na hiyo ni kutokana na klabu hiyo kuyumba kiuchumi hasa ukizingatia haina mdhamini baada ya kujitoa kwa waliokuwa wadhamini Kilimanjaro.
Simba baada ya kuwapata nyota hao imeamua kuwaacha wachezaji Vicent Angban raia wa Ivory Coast, Musa Ndusha kutoka DR Congo na pia imewatoa kwa mkopo wachezaji Amme Ali, aliyekwenda Kagera Sugar, beki Emmanuel Simwanza aliyepelekwa Majimaji na Malika Ndeule ambaye amerudi kwenye timu yake ya zamani ya Mwadui FC.
Yanga mabingwa watetezi wameonekana kutumia hesabu nyingi baada ya kusajili wachezaji wawili kwa kuhofia kutovuruga kikosi chao ambacho kina malengo ya kucheza fainali ya Afrika mwaka ujao.
Yanga imemsajili Justine Zullu kutoka Zesco United na Emmanuel Martin kutoka JKU ya Zanzibar usajili wote huu ukiwa umetumia kiasi kidogo zaidi cha pesa ambacho ni milioni 150 ukijumuisha na mishahara ya nyota hao.
Klabu ya Mbeya City mbali ya kumsajili Ngassa pia nayo imeshika nafasi ya nne kwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa kufanya usajili kuimarisha kikosi chao.
Viongozi wa timu hiyo hawajaweka wazi figa kamili ya kiasi kamili walichokitumia lakini inakadiriwa inafika milioni 250 za Kitanzania na kwa mara ya kwanza inaingia kwenye orodha ya timu tano bora zenye kijiweza kifedha baada ya ya Azam, Yanga na Simba.
Katika kipindi hiki cha dirisha dogo wachezaji waliosajiliwa na Mbeya City ni Tsipa Leonard kutoka Caps United ya Zimbabwe, Tito Okello, Hood Mayanja pamoja na beki William Otong wote raia wa Uganda na mzunguko wa kwanza alichezea African Lyon.
Kagera Sugar haimo kwenye orodha ya klabu hizo tano zilizotumia kiasi kikubwa cha pesa lakini nayo imejitutumua kwa kufanya usajili wa nyota kadhaa kwenye dirisha dogo.
Kocha Mecky Maxime ameweza kumsajili kipa mkongwe Juma Kaseja, aliyekuwa mchezaji huru na beki Mohamed Fakhi, kutoka JKT Ruvu na  Amme Ali ambaye amekwenda kwa mkopo kutoka Simba.
Timu ya Majimaji yenyewe imeimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili Kelvin Sabato kutoka Stand United na pia imempokea beki Emmanuel Simwanza kutoka Simba na kipa Kuitche Bidou raia wa Ivory Coast.
Kikosi cha Mwadui FC, baada ya kufanya vibaya mzunguko wa kwanza mzunguko wa pili kimepania kubadilika ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zake wakiwa chini ya kocha Ally Bushiri,
Timu timu imesajili nyota watano wapya ili kurekebisha hali mbaya ya kushuka daraja ambayo inawanyemelea.
Nyota wapya waliotua kwenye kikosi hicho cha kocha Bushiri ni  alisema Awadh Juma na Malika Ndeule wote  wakitokea Simba kwa mkopo, wengine ni Razack Khalfan(Singida united),Abdallah Seif(Azam) na Meshack Abea(African Lyon).

About Good Sensei

Good Sensei
Recommended Posts × +

Entertainment

Latest News

Pictures